USHAWAHI KUKUTANA NA CHUO KINACHOTOA DEGREE YA BANGI?, KIFAHAMU HAPA

Image result for northern michigan university weed
Unaambiwa chuo kikuu cha NORTHEN MICHIGAN huko Marekani, kinatarajia kuanzisha kutoa mafunzo ya Degree kwa Somo la Bangi.
Image result for WEED
Kupitia taarifa ambayo imetolewa na FOX NEWZ, imefunguka kwamba Chuo cha NORTHEN MICHIGAN kimeamua kutoa mafunzo ya levo ya Degree kwa wanafunzi ambao wanatamani kujishughulisha na kilimo pamoja na uuzaji halali wa bangi kwa ajili ya kujipatia fedha kama zilivyo biashara zingine.

Moja ya maprofesa ambao watahusika kufundisha somo hilo, Brandon Canfield, amedai kwamba, ili  mwanafunzi aweze kufanikiwa na kufaulu katika somo hilo, atahitaji vitu viwili vya muhimu ambavyo ni KUJITOLEA pamoja na KUHAMASIKA, anadai kwamba humo ndani hapatakuwa rahisi, kutokana na mwanafunzi anapaswa kufahamu kwa ufasaha Zaidi Biology, Botany, Marketing, Finance, Horticulture pamoja na Chemistry vizuri.

Profesa huyo aliendelea kufunguka kusema kwamba, Wanafunzi hawatopanda Bangi madarasani, ila watapanda maua mengine yenye ufanano sawa na Bangi na yanayoweza kusaidia katika swala zima la madawa ya kutibu.

Mpaka sasa tayari kuna jumla ya wanafunzi 12 ambao wamejiunga na Program hiyo.

0 comments:

Post a Comment