FAHAMU FAIDA ZA KUCHEZA GAMES

Wewe ni mchezaji mzuri wa Games? Kila mda huwa unapenda kucheza games haijalishi wewe unatumia Smartphone, Computer, Playstation, Xbox au kingine chochote kile ambacho huwa unatumia Kucheza Games, kuna watu wengine wanapenda Soccer, Action au Racing haijalishi, sasa fahamu faida unazopata unapokuwa unacheza Games.


1:FAIDA YA KWANZA INAFANYA UBONGO WAKO UNAKUWA ACTIVE

Baadhi ya tafiti zilizofanywa na Wajerumani zinaonyesha kuwa mtu anayependelea sana kucheza Games kama Super mario na Game zingine za Mission huwa ubongo wake unakuwa uko vizuri kwenye kufikiri na kuchanganua mambo ambayo yanamzunguka katika jamii.



2:AKILI YAKO INAKUWA HAIZEEKI

Kutokana na tafiti zilizofanywa na chuo cha Lowa kinasema kuwa kucheza game ndani ya Masaa matano kila siku inafanya akili yako kuwa na uwezo wa haraka wa kufikiri.



3:KUBORESHA MACHO YAKO KUONA ZAIDI

Hii husaidia macho yako kuweza tambua kitu chochote kwa haraka zaidi, iwe kwenye giza au mahala popote, uwezo huo unafanya ubongo na wenyewe kuwa unafanya kazi kwa haraka zaidi, Tafiti zilizofanywa zinasema kuwa huwa kwa wale wanajeshi macho kuweza kuwa na haraka ya kutazama vitu kwa kasi bila kupoteza taswira ya jambo husika, 




4:HUSAIDIA KUPUNGUZA MAWAZO

Mbali na kutumia pombe au madawa ya kulevya kwa vijana, Game zinapunguza mawazo na bila kukuletea madhara yeyote yale, hii ni kutokana na Tafiti zinazofanywa Nchini Marekani kuhusu Vijana ambao wanatumia madawa ya kulevya kupunguza mwazo, walichukuliwa na kuwekwa katika Game ili kupunguza mawazo yao.



0 comments:

Post a Comment