MENEJA WA ALIKIBA AZUNGUMZIA USHINDI WA TUZU YA MTV EMA

Image result for alikiba
Zilitufikia taarifa siku ya jana kutoka katika uongozi wa msanii  Alikiba kuhusiana na lile sakata la tuzo ya MTV Europe Music Awards (EMA) katika category ya Best African Act ambayo hapo awali alikabidhiwa Wizkid kimakosa wakati mshindi halali wa tuzo hiyo ni Alikiba.
Na taarifa hizo zilikuwa za majibu mazuri kutoka MTV kuwa ni kweli Alikiba ndiye mshindi halali wa tuzo hiyo na hivyo ikaripotiwa kufanya utaratibu wa kumnyang’anya tuzo hiyo Wizkid na kuhakikisha wanamkabidhi Alikiba.
Meneja wa Alikiba Ndg. Seven Mosha ambaye alitoa ufafanuzi ni jinsi gani makosa yalitendeka katika utoaji wa tuzo hiyo.
“Kuna vitengo viwili, MTV Europe na MTV Africa, kosa inaonekana kwamba lilitokea upande wa MTV Africa, na hata ukiangalia taarifa za Wizkid kushinda tuzo hiyo zilitokea katika mitandao ya MTV Africa na kwa upande wa MTV Europe walikuwa hawajatangaza mshindi wa hiyo category. Na hata system ya MTV Europe ilikuwa ikionyesha kuwa mshindi ni Alikiba.” Alisema Seven Mosha.

0 comments:

Post a Comment