WENGER AAPA KULIPA KISASI WIKIENDI HII..!!


Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amesema kuwa mechi ya Ligi ya Uingereza dhidi ya Swansea City ni fursa nzuri ya kupima maendeleo ya kikosi chake kulinganisha na msimu uliopita.

Washika bunduki wa London wataikaribisha Swansea katika uwanja wa Emirates wikiendi hii jumamosi wakitaka kulipiza kisasi cha kipigo cha 2-1 cha msimu uliopita.

Ni matokeo yaliyozima tumaini la Arsenal la ubingwa, na Wenger amekitaka kikosi chake kuonesha ubora wao msimu huu kwa kukabiliana na presha ya kuwa washindani.
"Mwaka jana tulikabiliwa na mazingira magumu sana dhidi ya Swansea ambao waliua fursa yetu ya kutwaa ubingwa Ligi Kuu," Wenger alikiambia beIN Sports.

"Tunayo fursa nzuri kuonesha kuwa tulijifunza kutoka kwenye makosa yetu na kwamba tunao uwezo wa kushughulika na wapinzani wa aina hii. Hilo ndilo jukumu letu. Tunahitaji kujituma kwa sababu wachezaji hawakuwepo na hakuna aliyekuwepo hapa.
"Ni lazima tuoneshe uwezo wetu kwamba tunaweza kushughulika na mechi kama hizi tukiwa na nafasi kubwa ya kushinda. Tulishindwa kufanya vizuri msimu uliopita na tunataka kuonesha kuwa tunaendelea mbele."

Mechi hiyo pia itakuwa ya kwanza kwa Bob Bradley tangu alipokabidhiwa mikoba ya kuinoa Swansea.

0 comments:

Post a Comment