RONALDO ANATAMANI HIKI KWA KIUNGO WA LIVERPOOL, COUTINHO


Image result for coutinho
Mshindi wa Kombe la Dunia  Ronaldo amekiri kuwa angependa kumuona kiungo wa Liverpool Philippe Coutinho akicheza Real Madrid.
Nyota huyo, 24, amekuwa akifanya vizuri tangu alipotua Anfield kwa majogoo wa jiji  akitokea Inter Milan mnamo 2013, tetesi zikipamba moto kuwa Barcelona au Paris Saint-Germain zinaitaka saini yake.

Hata hivyo, Ronaldo anataka kumwona Mbrazili mwenzake Coutinho - ambaye ana mkataba na Liverpool hadi 2020 - akihama meli na kujaribu maisha mengine na wachezaji bora wa La Liga wanaokipiga Real Madrid.

"Ningependa kumwona Coutinho Real Madrid," aliiambia redio ya Hispania Onda Cero. "Soka la Hispania, bila shaka, ni bora katika historia.

Wamekuwa wakinunua wachezaji bora na kuzalisha soka lenye mvuto zaidi."
Ronaldo amecheza miaka mitano Santiago Bernabeu, akifunga mara 104 katika mechi 177 Real Madrid na kuiwezesha timu yake kutwaa mataji mawili Hispania.

0 comments:

Post a Comment