Tukiwa tunaelekea kwenye mechi kati ya Tanzania na Nigeria, Kocha Mkuu wa Taifa Stars amefanya mabadiliko ya wachezaji wake.
Kocha mkuu wa Taifa Stars, Charles Mkwasa amewaanzisha Mohamed Hussein na Shiza Kichuya katika kikosi cha Taifa Stars kitakachoivaa Nigeria.
Kichuya amemtoa Farid Musa katika kikosi cha kwanza huku Hussein akimweka benchi mlinzi wa pembeniMwinyi Haji.
Kikosi kamili: Aishi Manula, Shomari Kapombe,Mohamed, Andrew Vincent, David Mwantika, Himid Mao, Jonas Mkude, Simon Msuva, John Bocco, Mbwana Samatta.
Akiba: Said Kipao, Mwinyi Haji, Ibrahim Jeba, Yassin Mzamiru, Ibrahim Ajibu, Farid Mussa, Juma Mahadhi.
0 comments:
Post a Comment