SIASA: MH. MAGUFULI AMETISHIA KUBADILI NOTI YA TSH?

Mh. john joseph Magufuli leo ametishia watanzania huenda akabadilisha fedha ya tanzania noti ya shilingi elfu 10,000.

Katika kile kinachoonekana kutaka kuwadhibiti watu wanaodaiwa kuficha fedha, mheshimiwa Magufuli amesema kwa mamlaka aliyonayo anaweza kuamua kubadili fedha ili zile zinazofichwa na watu hao wakose mahali pa kuzipeleka.

Akizungumza katika mkutano wa 14 wa mwaka wa wahandisi uliofanyika katika ukumbi wa Mlimani City Dar es salaam  leo mchana, Magufuli amesisitiza kuwa kauli hiyo ni mahsusi kwa watu walioficha fedha katika majumba yao na kuwahamasisha kuachana na tabia hiyo ili fedha hizo ziingie katika mzunguko wa pesa .

Huku akisisitiza kuwa katika utawala wake fedha za bure hazitakuwepo kwa sababu zilizokuwepo awali zilitokana na fedha za wizi kutoka serikalini ambazo kwa sasa zimedhibitiwa, alisema kwa mwendo anaokwenda nao sasa ni ngumu kwa mwananchi kupata fedha bila kufanya kazi.



source: Mwananchi






0 comments:

Post a Comment