MAZITO YA NAY WA MITEGO KWA SHAMSHA FORD

Image result for shamsa ford na ney wa mitego
Hakuna asiyejua kama mwanadada wa Bongo Movie Shamsa Ford na rapper Nay wa Mitego kwamba walikuwa katika mahusiano ya kimapenzi hapo awali.
Mwanadada huyo hapo jana ameweza kufanikiwa kutimiza nusu ya dini kwa imani ya dini yake kwa kufunga pingu za maisha (Ndoa) na mfanya biashara maarufu wa nguo jijini Dar es Salaam Chidi Mapenzi.
Kama ilivyo kawaida kwa mtu yeyote hali inakuaga sio nzuri pale mtu ambaye ulikuwa naye katika mahusiano anapoamua kupiga hatua na kufanya maamuzi magumu kwa kufunga ndoa na mtu mwingine bila kujalisha kwamba mwanadada Shamsa Ford na Nay wa Mitego walikwisha utangazia umma kwamba wao hawapo tena kwenye mahusiano na kilichobaki ni urafiki wa kawaida tu.
Na hicho ndicho kiliwasukuma watangazaji wa kipindi cha D’Wikend Chatshow cha Clouds TV Qwhisar naSoudy Brown kumpigia simu Nay wa Mitego na kutaka kumjulia hali yake. Na hiki ndicho alichokisema Nay wa Mitego.
“Namtakia kila la kheri lakini wakiachana atarudi tu. Hatuombi waachane lakini kuna hapa na pale inaweza kutokea endapo wakishindwana me ntampokea kwa mikono miwili.”
Dondosha neno moja tu kwa Nay wa Mitego kwa uamuzi wake huo ambao kauchukua.

0 comments:

Post a Comment