ALAMA MPYA ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI KUANZA KUTUMIKA



Serikali imetangaza rasmi juu ya matumizi ya alama mpya za jumuiya ya afrika mashariki zitazo tumika kwenye shughuli zote za serikali na ofisini.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Mindi Kasiga amezitaja alama hizo kuwa ni bendera ya Taifa, bendera ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, wimbo wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki na wimbo wa Taifa.

“Mkataba huu unasisitiza jumuiya hii kuwa jumuiya ya watu, hivyo watanzania watahusishwa katika hatua zote za mtangamano huo, pamoja na kushirikishwa kikamilifu katika hatua mbalimbali za jumuiya ili kujua madhumuni ya kunufaika na fursa mbalimbali zitakazaopatikana ndani ya Jumuiya hiyo”,

alama hizo zimeanziswa ikiwa ni hatua ya utekelezaji wa Mkataba wa uanzishwaji wa jumuiya hiyo kifungu cha 7(a).

Vilevile, taasisi binafsi  zinaweza kutumia alama hizi, huku shule na vyuo vikisisitizwa kutumia alama hzi kama sehemu ya kuelimisha na kuhamasisha vijana kuhusu Jumuiya ya Afrika ya Mashariki. Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inaratibu upatikanaji wa sampuli ya alama hizo kwa gharama za taasisi, wizara au Ofisi husika.

SOURCE:millard

0 comments:

Post a Comment