KESI YA WATUHUMIWA WA KOSA LA UBAKAJI BINTI MIAKA 21, KUSIKILIZWA TENA JUNE 1 MWAKA HUU

13166801_1632014527124402_853971816_n

Watuhumiwa wa kosa la ubakaji na udhalilishaji wa msichana wa umri wa miaka 21 huko mkoani Morogoro, Jana jumatano walipandishwa kizimbani Mahakani mkoani humo.

 Idd Adam Mabena wa Njombe, Zuberi Thabiti wa Mbarali wanadaiwa kutenda kosa hilo April 27 usiku kwenye nyumba ya kulala wageni. Hata hivyo washtakiwa hao wamekana makosa yao na hivyo kesi hiyo itasikilizwa tena June 1.

Upande wa mashtaka pia umewasilisha kiapo cha pingamizi la dhamana kwaajili ya usalama wa washtakiwa hao kutokana na tukio lao kugusa hisia ya jamii.


0 comments:

Post a Comment