Moja kati ya ma Director chipukizi wanaofanya vizuri kwenye ulimwengu wa uongozaji video hapa Bongo ni kijana Deo abel.
Tasnia hii ya uongozaji video imekuwa na changamoto nyingi sana haswa kwa wanaochipukia lakini director Deo abel ameonesha kuwa uvumilivu, jitihada na kuipenda kazi yako ndiyo itakayo kuweka on top.
Baada ya kufanya vizuri na video zake Baishoo(almasi masound) na Nikilewa(Nasi ft shaa) safari hii amevuka mipaka na kufanya kazi na msanii kutoka Burundi anayeishi nchini Marekani.
Video ya wimbo inaitwa Korokokoya imefanywa na msanii Babbi kutoka burundi anayeishi Marekani, ndani ya video kuna maeneo mawili tofauti ambayo ni Bongo pamoja na Marekani San francisco.
0 comments:
Post a Comment