DAR ES SALAAM WATUMISHI HEWA WAFIKIA 209

Makonda

 Wakuu wa idara za mkoa na manispaa wametia saini na kula kiapo kuwabaini bila kuficha ukweli kuhusu watumishi hewa kwa Mkoa wa Dar es Salaam wakiongezeka na kufikia 209.

Awali, mkoa huo ulibainika kuwa na watumishi hewa 17.


Hivi karibuni, Mkuu wa mkoa huo, Paul Makonda alisema wamebaini watumishi hewa 209 ambao wameisababishia Serikali hasara ya Sh 2.9 bilioni.

“Awali wakuu wa Idara hao walihakiki watumishi hewa 17 ambao waliingizia (Serikali) hasara ya Sh330 milioni. Baada ya kuwabana maofisa hao tumepata watumishi hewa 209 ambao walilipwa Sh2.9 bilioni, kutokana na hili nimetoa wiki moja wawe wamekamilisha kuhakiki,” alisema Makonda.

0 comments:

Post a Comment