
Klabu kongwe na zenye upinzani Tanzania, leo Februari 20 Simba na Yanga wanakutana Dimbani katika mchezo wa marudiano wa mzunguko wa pili wa ligi Kuu Tanzania Bara katika Uwanja wa Taifa Dar es salaam.
Mchezo huo ambao unatarajiwa kujaza mashabiki wengi uwanjani siku ya leo, Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania (TFF) limetangaza kufunga Barabara hizi:
Kuanzia DUCE kuelekea uwanja wa Taifa Barabara hiyo itafungwa na kuwaomba mashabiki kutumia Barabara ya MANDELA kuingia uwanja wa Taifa kushuhudia mtanange wa leo kwa watani wa jadi.


0 comments:
Post a Comment