RAPPER JCB AMERUDI TENA NA "TURU JUU YA NGEU"

Rapper JCB kurudi upya na ngoma mpya kutoka katika Album mpya ya "Turu juu ya Ngeu" iliyofanya nchini Ufaransa.

Rapper huyo anayetokea Watengwa, alisikika katika kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio, akisema kuwa, ngoma hiyo itatoka pamoja na video akiwa amemshirikisha rapper Dishwaa kutoka Watengwa.

"Watengwa rekodi tunarudi upya katika television yako na radio yako, Tarehe moja November tutaachia ngoma kutoka katika Album ya 'Turu juu ya Ngeu' nimefanya na mwanangu Dwii na tumefanyia Ufaransa" Alisema JCB.

0 comments:

Post a Comment