JOKATE: USIVIMBE KICHWA BAADA YA KUPATA UMAARUFU

Kupitia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio, Mwanamitindo na muimbaji Jokate Mwegelo, amewataka wasanii kutumia umaarufu wao vizuri na kutovimba Kichwa pale wanapoona umarufu wao unakua ili kuepukana kuwa na mwisho mmbaya na ili kuweza pata ushirikiano na watu mbalimbali katika kazi.

"Unjaua ukiwa maarufu alafu mtu anakuwa anaimba nyimbo zako,unaanza kuvimba kichwa na kusahau kuwa kuna watu walikuwepo na walihit kama wewe,hii ni cycle kwamba leo umehit,kesho yule"Alisema Jokate

"Wanatakiwa kujua kwamba sio kwamba watakuwa juu milele, hiyo haipo, cha muhimu ni kufanya kazi kwa heshima hasa kwa wale ambao wapo kwenye Industry" Alisema Jokate

0 comments:

Post a Comment