KAMA NIMEJIANDIKISHA MKOA MWINGINE NA KURA NATAKA NIPIGE DAR ES SALAAM INAWEZEKANA?

Kwa wale mtakuwa na maswali mengi ya kujiuliza, endapo mimi nimejiandikisha Morogoro au mkoa mwingine mbali na Dar es salaam, alafu kwenye kupiga kura nahitaji kupigia nyumbani Dar es salaam?

Sasa mkurugenzi

wa huduma za kisheria wa tume ya Uchaguzi,Emmanuel Kawishe. anatuambia kuwa

"Mtu atapigia kura mahali ulipojiandikisha kama ulijiandikisha Dar es Salaam hakikisha unarudi kuja kupigia kura Dar es Salaam  kwa hiyo hatoruhusiwa mtu kwa mujibu wa sheria kupigia kura sehemu yoyote kifungu  cha 91 kifungu kidogo cha tatu A kinasema mtu ataenda sehemu ya kujiandisha na kuruhusiwa kupiga kura’ – Emmanuel Kawishe

‘Kwa hiyo kama mtu akiwa Dar es Salaam labda amejiandikisha Arusha anachotakiwa ni kufanya maamuzi ya kwenda Arusha kwenda kituo alichojiandikisha ndipo aweze kushiriki kupiga kura’ – Emmanuel Kawishe

0 comments:

Post a Comment