Watanzania wote kwa ujumla tuungane na kuhamasisha amani katika kipindi hiki cha uchaguzi ili kuendeleza amani inayotujengea sifa kubwa sana kila kona ya dunia.
Habarika imechukua fursa hii kukuasa ewe kijana,dada,baba,mama, bibi na babu kutojihusisha na vitendo vyovyote vya uvunjifu wa amani na kukuomba kuungana kwa pamoja ili kuweza kuhubiri amani ilituweze kulinda umoja wetu na Amani.
Tunatambua kila mtanzania anaitikadi yake hasa katika vyama vya siasa hivyo hatupaswi kuchukiana wala kutengana kisa tu itikadi au upenzi unatofautiana tunawaomba watanzania kuweka itikadi pembeni na kuungana kudumisha amani katika nchi yetu.
Tulianza kwa pamoja tukiwa na amani iliyo tujaa mioyoni mwetu hatukujali kabila,dini,umri,jinsia,wala rangi na tukauanza safari pamoja vivyo hivyo pia tunapaswa kuwa pamoja kama tulivyo anza ili tuweze kukubariana na matokeo na kuupokea uongozi mpya wa Tanzania wa awamu ya Tano.
Tukumbuke kuwa hiki ni kipindi cha mpito na kisitufanye au kututenganisha mwishoni tutamaliza uchaguza na tutaendelea na maisha tukapige kura tukiitanguliza amani kwanza Mungu ubariki uchaguzi mungu ibariki Tanzania.
0 comments:
Post a Comment