DIAMOND PLATNUMZ KUCHUANA NA PRIYANKA CHOPRA

Bado Diamond platinumz anakipengele kizito mbele yake, hii ni baada ya kunyakua tuzo ya MTV EMA#BEST AFRICAN ACT. anaelekea kwenye tuzo zingine ambazo zinamkabili mbele yake ni ya BEST WORLD WIDE ACT:AFRICA/INDIA. ambako anakutana na mwanadada machachali sana kwenye tasnia ya uigizaji wa filamu na uimbaji, Priyanka Chopra.


Mwanadada priyanka ambaye kwa sasa amekuwa gumzo sana huko india, kwa sasa anatamthilia ambayo anacheza inaitwa "QUANTICO" ambayo inarushwa na luninga ya ABC.

Diamond platnumz anaitaji kura nyingi sana kutoka kwa wa Tanzania wenzake na kwa Africa nzima ili kuweza kufanikisha kuwa kidedea wa tuzo hiyo ya Best Worldwide Act:India/Africa.

Tuzo hizo ambazo zitatolewa tarehe 25 Oct 2015 ambapo watatangaza mshindi ni nani na pia kuorodhesha na washindi wengine kutoka mabara tofauti.

0 comments:

Post a Comment