BONGO STAR SEARCH 2015 WINNER NI KAYUMBA JUMA

Kayumba Juma ni mshiriki aanayetokea Temeke jijini Dar es salaam, ameibuka kidedea kwenye shindano la BSS kwa kuondoka na shiling milioni 50 jana kwenye ukumbi wa King solomon.

Kayumba ambaye ndio mshindi wa shindano hilo la BSS pamoja na wenzake walioingia hatua ya fainali walipata shavu la kusimamiwa kazi zao za muziki na TipTop connection kwa mwaka mmoja.

Mshindi wa tatu alikuwa ni Farida na wapili ambaye alikuwa akienda sambamba na Kayumba ni Nasib Fonabo.

Mizunguko yote ilikuwa migumu na washiliki wote walikuwa wako vizuri, mpka kufikia hatua ya top two kati ya Kayumba na Nasib bado wote walikuwa wanatisha.

Kayumba aliwaamsha mashabiki wengi baada ya kuja na staili ya tofauti kwa kuimba wimbo wa Isha mashauzi na ndio uliompelekea kuchukua ushindi huo, huku Nasib aliimba wimbo wa Ed sheeran.


kayumba akiwa amekumbatiana na Penny


Kayumba akiwa na mwenzake Nasib


Kayumba akishangilia baada ya kutangazwa ndiye Mshindi wa BSS

0 comments:

Post a Comment