VANESSA MDEE AAMUA KUFANYA JAMBO HILI KWA WANAFUNZI


Image result for Vanessa mdee
Mwishoni mwa wiki iliyopita, Tanzania na Dunia nzima ilizizima kwa simanzi kutokana na ajali iliyotokea mkoani Arusha ikihusisha vifo vya Wanafunzi 32, Walimu 2 na dereva aliyekuwa akiendesha school bus hilo.
Ajali ambayo iliwagusa wengi hususan Wanafunzi kwakuwa wameondokewa na wenzao ambao wengi wao walikuwa na malengo na ya kufika mbali zaidi na pengine kuja kulisaidia taifa kwa namna moja ama nyingine.
Mwanadada Vanessa Mdee ameamua kujumuika na Wanafunzi na kuwatia moyo katika kipindi hiki kigumu, ndipo ambapo aliamua kutembelea Jangwani Secondary School hapo jana May 9.
Kupitia ukurasa wake wa instagram, Vanessa Mdee aliandika Leo nilipata nafasi ya kuwatembelea wanafunzi wa Shule ya Jangwani. Ilikuwa nafasi ya kipekee na nawashukuru sanaaaa walimu wao kwa kunipa fursa hii. Ni muhimu sana kuwa kumbusha kwamba tuko nao sasa wakati huu mgumu na pia siku zote. These lil ladies are the future. đź’ś.

0 comments:

Post a Comment