Klabu ya Simba hii leo imemtambulisha kocha wake raia wa Cameroon Joseph Marius Omog ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu hiyo.
Rais wa Simba Evance Aveva amesema, wamekuwa katika kipindi kirefu cha kutafuta kocha na wamefanikiwa kumpata Omog kwa kutumia vigezo ambavyo wanaamini ataifikisha timu pale wanapopatarajia.
Omog amewasili Tanzania kwa mara ya pili ambapo kwa mara ya kwanza 2014 aliwasili nchini ambapo aliifundisha klabu ya Azam FC kwa msimu mmoja na nusu na alifanikiwa kuipa taji la Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara kwa mara ya kwanza.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Simba ambaye naye ametambulishwa hii leo, Patrick Kahemele amesema, lengo lake katika klabu hiyo ni kuhakikisha Simba inarudi katika hali ya mafanikio iliyokuwa nayo hapo awali.
Kahemele amesema, kila klabu inalengo la kupata ushindi kwa kila michuano na kwa upande wake pia atahakikisha Simba inabadilika na kurudia enzi zake za kutwaa ubingwa.
0 comments:
Post a Comment