NEYMAR ASAINI MKTABA MPYA WA KUITUMIKIA BARCELONA


Mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil na Barcelona, Neymar amesaini mkataba mpya wa miaka mitano wa kuendelea kuitumikia Barcelona mpaka 2021.
Neymar amefunga mabao 55 katika michezo 93 za La Liga tangu alipojiunga na klabu hiyo akitokea Santos kwa ada ya paundi milioni 48.6 mwaka 2013.
Pia mshambuliaji huyo alifunga mabao 46 katika mechi 70 kwa nchi yake.
Klabu za Manchester United na Paris St-Germain wote walikuwa wakiripotiwa kuwa wamevutiwa na mshambuliaji huyo Mbrazil mwenye umri wa miaka 24.
Barcelona walilazimishwa kulipa faini ya pauni milioni 4.3 mwezi Juni kufuatia makosa yaliyofanyika katika uhamisho wa Neymar kutoka Santos.

0 comments:

Post a Comment