Bunge limetengua kanuni zake na kubadilisha muda wa kumaliza shughuli zake kwa lengo la kuruhusu wabunge Waislamu kutimiza wajibu wao wa kiimani katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Utenguzi wa kanuni hizo ulipitishwa jana baada ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Bunge, Jenister Mhagama kuomba Kanuni ya 28(4), ambayo kwa ujumla wake inaelekeza kwamba Bunge litaendelea kukaa hadi saa 2:00 usiku.
Mhagama aliomba kanuni hiyo itenguliwe na badala yake, kuanzia siku ya kwanza ya Ramadhani, Bunge lirejee saa 10:00 alasiri kama ilivyo sasa na kuahirishwa saa 12:00 jioni. Hoja hiyo iliungwa mkono na wabunge wote waliokuwamo ndani.
0 comments:
Post a Comment