WHATSAPP YAFUNGIWA KWA MARA NYINGINE BRAZIL

WhatsApp-4

Mtandao maarufu zaidi Duniani wa Whatsapp umefungiwa tena nchini Brazil kwa mara nyingine.

Hakimu mmoja nchini Brazili amefunga mawasiliano ya mtandano wa simu kwa njia ya whatsapp kwa saa 72.
Hakimu huyo Marcel Montalvao amesema kampuni inayomiliki mtandao huo imeshindwa kusaidia kutoa taarifa katika kesi ya uhalifu.
Wamiliki wa mtandao huo wa Whatsapp ambao pia wanamiliki mtandao wa Facebook wamesema kuwa wamekatishwa tamaa na kitendo hicho kwa kuwa wamekuwa wakitoa ushirikiano wa kutosha mahakamani.

Mtandao huo umekuwa ukifungiwa mara kadhaa nchini Brazil kwa miezi michache ya karibuni kwa sababu zinazofanana na hizo.

0 comments:

Post a Comment