Tulijiunga kwa kutumia simu za Android,Apple,Symbian,Windows phone na Nokia S40, lakini sa hivi hata ukiwa na Windows desktop au Mac pia unaweza kutumia Whatsapp.
Whatsapp imezidi kujiongeza na safari hii wametuletea huduma hiyo katika komputa yako, naamanisha unaweza kutumia whatsapp katika komputa yako.
Huduma hii mpya haina utofauti na ile Whatsapp web ambayo ilianzishwa januari mwaka jana 2015.
Ili uweze kutumia whatsapp kwenye komputa yako ni lazima iwe na uwezo kuanzia Windows 8 na kuendelea na kwa upande wa Mac lazima iwe Mac OS 10.9 na kuendelea ili kuweza kufurahia huduma hiyo mpya.
Kwa sasa whatsapp katika komputa yako haina huduma ya voice call ila huduma zingine zinazopatikana katika simu unazikuta kama kawaida.
0 comments:
Post a Comment