SNURA AMESAJILIWA RASMI KWENYE SHUGHULI ZA KISANII NA AMEOMBA RADHI KWA VIDEO YA CHURA

snura

Msanii Snura Mushi ambaye wimbo wake wa Chura ulipigwa marufuku na serikali ya Tanzania ameomba radhi na kuahidi kutekeleza maagizo ya serikali.

Muimbaji huyo amekutana na waandishi wa habari Alhamis hii kwenye ukumbi wa Habari Maelezo jijini Dar es Salaam.



Kwenye mkutano huo na waandishi wa habari, Snura amedai kuwa tayari amekamilisha mchakato wa usajili na BASATA imempa kibali. Pia amedai kuwa amewasilisha video mpya ya wimbo huo kwa bodi ya filamu ya Tanzania ambayo itaikagua.

index

Snura
Snura amesema amechukua hatua na kusajiliwa rasmi kwa ajili ya shughuli za kisanii.

0 comments:

Post a Comment