RAISI MAGUFULI ASHUSHA KODI YA MAPATO KWA WAFANYAKAZI



Rais John Magufuli ameshusha kodi ya mapato ya mshahara (paye) kwa wafanyakazi kutoka asilimia 11 mpaka asilimia tisa. Rais Magufuli alitangaza punguzo hilo leo mjini Dodoma alipokuwa akihutubia kwenye siku ya wafanyakazi duniani ambayo kitaifa imefanyika Dodoma.
Amesema wafanyakazi wamekuwa waaminifu katika kulipa kodi ambayo inachangia kwenye maendeleo ya taifa kupitia mishahara yao. Alisema kwa kuwa bado vita dhidi ya wafanyakazi hewa na ufisadi inaendelea, ataangalia namna ya kuboresha mishahara yao hapo baadaye.

"Niliwahidi wakati wa kampeni zangu kuwa nitapunguza kodi ya mapato kwenye mishahara yenu, sasa natamka kuwa nashusha kodi leo toka asilimia 11 hadi asilimia 9, najua punguzo hilo litakuwa limeacha pengo ya serikali, lakini tutangalia vyanzo vingine vya mapato vya kujazia hapo"Alisema Raisi Magufuli.



0 comments:

Post a Comment