Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson amesema kuanzia Jumatatu, wataanza kutumia mfumo wa kielektroniki (biometric) kuchukua alama za vidole za wabunge na wageni waingiao bungeni sambamba na kujaza fomu za usajili wa majina.
Dk Tulia amesema kutakuwa na sehemu nne zitakakofungwa mashine za usajili kwa wabunge na watu wengine.
Amesema fomu zilizokuwa zikitumika kujiandikishia awali, hazitatumika tena.
Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah amesema utaratibu huo unalenga kuimarisha usalama kwa sababu watu wanaoingia ukumbini hapo kila siku ni kati ya 1,000 hadi 2,000.
0 comments:
Post a Comment