Muungano wa upinzani CORD umekuwa ukifanya maandamano Jumatatu kila wiki kuwashinikiza maafisa wakuu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (IEBC) wajiuzulu.
Mashirika ya kutetea haki za kibinadamu nchini Kenya yameshutumu maafisa wa polisi wakisema walitumia nguvu kupita kiasi kukabili waandamanaji jijini Nairobi Jumatatu.
Tume ya Taifa ya Haki za Kibinadamu (KNHRC) imesema imeshangaza sana na video na picha ambazo zinaenea kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari kuhusu yaliyojiri wakati wa maandamano hayo.
Picha hizo zinawaonesha polisi wakiwakabili waandamanaji kwa marungu.
Baadhi ya wakenya mtandaoni pia wamekuwa wakiwashutumu maafisa wa polisi na kitambulisha mada #StopPoliceBrutality (Komesha Ukatili wa Polisi) kinavuma Kenya.
Mamlaka huru ya kiraia inayofuatilia shughuli za polisi (IPOA) pia imeshutumu vitendo vya maafisa wa polisi na kusema walivuka mipaka.
SOURCE:BBC
SOURCE:BBC
0 comments:
Post a Comment