Marcus Rashford amesaini mkataba mpya wa miaka minne wa kuendelea kuitumikia Klabu yake ya Manchester United.
Mkataba huo mpya wenye kipengele cha kuongeza mmoja zaidi na ambao utafikia tamati mwaka 2020 utamuingizia nyota huyo mwenye miaka 19 kitita cha £25,000 kama mshahara wake wa wiki.
Baaada ya kusaini mkataba huo Rashford alikuwa na haya ya kusema
" Nimefurahi kusaini mkataba mpya.Daima nimekuwa shabiki kipenzi wa Manchester United,kupata nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza ni ndoto iliyotimia.Nashukuru kwa kupata nafasi ya kuonyesha kipaji changu.Kupata nafasi ya kucheza katika klabu kubwa duniani ina maana kubwa sana kwangu na kwa familia yangu.
"I am delighted to have signed a new contract. I have always been a Manchester United fan, so to be playing in the first team really is a dream come true. I am grateful for having the chance to prove myself. To be able to play football at the biggest club in the world means everything to me and my family"
Mwingine aliyesaini mkataba mpya ni mlinzi wa kushoto Cameron Borthwick-Jackson,19. Nimekulia Manchester United na nimefurahia kila dakika niliyokuwa hapa.Msimu uliopita ulikuwa mzuri sana kwangu na jambo jema sana kwangu na kwa familia yangu.Nitaendelea kujituma na kupokea ushauri toka kwa kocha na benchi lake la ufundi.
“I have grown up at United and have enjoyed every minute of being here. Last season was an incredible experience to make my first team debut and a dream come true for myself and my family. I feel it stands me in good stead for continuing my development as a Manchester United player. I will continue to work hard and take advice from the manager and his coaching team to improve with every training session.”
0 comments:
Post a Comment