KAMATI YA MAADILI,HAKI NA MADARAKA YA BUNGE IMEWAFUNGIA WABUNGE SABA

Kamati ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge imewatia hatiani wabunge saba kwa makosa mbalimbali ikiwemo kudharau madaraka ya bunge. Wabunge Easther Bulaya naTundu Lissu wameadhibiwa kutokuhudhuria vikao vilivyobaki vya mkutano wa tatu na vikao vyote vya mkutano  wa nne.
Wabunge Pauline GekuHalima MdeeZitto Kabwe, Godbless Lema wasiudhurie vikao vyote vilivyobaki vya mkutano wa tatu na Mbunge John Heche hatahudhuria vikao kumi vya mkutano wa tatu. Makosa hayo waliyafanya mkutano wa pili mwezi January.

Huu ni uamuzi wa Kamati  ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge chini Mwenyekiti George Mkuchika (Mb).Wamekutwa na makosa mengi ya kukosa nidhamu na kutoheshimu Kiti Bungeni.

0 comments:

Post a Comment