MAADHIMISHO YA MZIKI WA JAZZ KWA MARA YA KWANZA NCHINI TANZANIA

Baraza la sanaa la taifa(BASATA) leo Mei 2 limefanya maadhimisho ya mziki wa Jazz ambayo yamefanyika katika kumbi za Baraza hilo maeneo ya Sharif Shamba jijini Dar es salaam.

Maadhimisho hayo ambayo yalisimamiwa na kikundi cha Jazz ambacho ni Tanzania Cultture Organisation(TCO) kinachoshughulika na tamasha la MARAHABA culture festival.

Wawasilishaji wa mada kuhusu mziki wa Jazz uliongozwa na John Kitime (Matumizi ya neno Jazz) na Kurwigira Maregesi (Historia ya Muziki wa Jazz) ambao wote kwa pamoja walielezea historia fupi juu ya mziki huu wa Jazz ambao ulianza katika kipindi cha mwaka 1947 kutoka nchi ya Congo ambapo wasanii wengi kutoka nchini Tanzania walikuwa wakielekea huko kwa ajli ya kurekodi na kusikika Afrika ya masharik kwa jumla.


Mziki wa Jazz ni mziki ambao hutofautiana na aina zingine za mziki kwasababu mziki huu huwa ni wakuita na kujibu(respond) ni mziki ambao unakuta vyombo vya mziki vinakuwa vikijibizana kwa ladha tofauti za Trumpet na Ngoma.


PICHANI NI KATIBU MKUU(BASATA) GODFREY LEDEJO MNGEREZA

0 comments:

Post a Comment