KIJANA WA MIAKA 10 AZAWADIWA $100,000 KWA KUDUKUA INSTAGRAM



Kijana wa miaka 10 ajulikanae kama JIN amepatiwa zawadi ya dola 100,00 kwa kuweza kudukua mtandao nguli wa jamii Instagram.

Jin aliweza kudukua mtandao huo mashuhuri kwa kuweza kufuta kila Comments ambazo yeye anaamua kuzifuta na haijarishi ni ya mtu mashuhuri au la. Kitu kilichofanya kuonekana wa pekee ni pale alipoweza  kufuta jumbe za mtandao huo wa Instagram ulipo post ujumbe wao kupitia mtandao huo.

“I would have been able to eliminate anyone,even Justin Bieber.”alisema Jani.

Jani alizungumzia pia kuwa hela hiyo ambayo ameipata ataweza nunua Baiskeli na vifaa vipya vya mpira na kikubwa anachopenda kuwa akiwa mkubwa ni kufanya kazi za ulinzi wa mtandao kupitia mtandao wa Facebook.
Sasa, ndiye mtu mchanga zaidi kutunukiwa pesa kwa kugundua udhaifu katika mitandao ya kampuni hiyo. Aliandikia wasimamizi wa mtandao huo barua pepe Februari kuwafahamisha kuhusu ugunduzi wake.

0 comments:

Post a Comment