Kampuni ya Zuri ilio na makao yake mjini Hong Kong imezindua rasmi simu aina ya Smartphone katika soko la Tanzania.Kampuni hiyo pia imeisajili kampuni ya DESPEC kama msambazaji rasmi wa simu hizo nchini Kenya Tanzania na Uganda.
Kulingana na gazeti la The Citizen nchini humo,uzinduzi huo uliofanyika mjini Dar es Salaam siku ya Jumatano unamaanisha kwamba simu za smartphone za Zuri kama vile C41,C42,C52 na S56 zinapatikana nchini Tanzania.
''Tumeona kwamba kuna fursa nzuri ya bidhaa zetu Tanzania...tunawasihi raia wa Tanzania kujipatia simu zenye ubora ili kukwepa gharama zinazokuja na simu baada ya kununua mbali na maswala mengine ya kiafya yanahuhusishwa na simu zenye kiwango cha chini',afisa mkuu wa simu za Zuri Bwana Vikash Shah,amesema.
Kulingana na The Citizen Tanzania,Mkurungenzi wa kampuni ya DESPEC Bw Riyaz Jamal anaamini kwamba kwa kuongeza Zuri katika soko la simu kutawasaidia raia wa Tanzania kupata simu zenye ubora na zilizo na bei ya chini.
''Wateja wanatafuta bidhaa za simu zilizo bora duniani,tunaamini kwamba Zuri itaturuhusu kupata mauzo mazuri nchini Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla'',alisema Jamal.
0 comments:
Post a Comment