WHATSAPP ENCRYPTION IMEKUWA NI HUDUMA BORA ZAIDI KATIKA ULIMWENGU WA APPLICATION ZA BURE

Whatsapp_Encryptio

Baada ya mtandao wa Whatsapp kuweka maboresho mapya ya ulinzi na usalama ya End to end Encryption, Kila kona ya Dunia imekuwa ikizungumzia juu ya Teknolojia hii inayopatikana katika ulimwengu wa App  za bure juu ya mtandao huu wa Whatsapp.

Kipindi cha nyuma Kampuni ya Apple iliingia katika mabishano makubwa na serikali ya Marekani pale walipotaka kuidukua simu ya Iphone ambayo ilitumika katika Uharifu na kusababisha Udukuaji katika simu hiyo, Whatsapp imeonyesha kutokubaliana na jambo hilo na kuamua kupiga hatua kubwa kwa watumiaji wake ambao ni zaidi ya Bilioni moja na kuwapa maboresho hayo ya faragha ambayo hayatoweza Dukliwa na Serikali,whatsapp na huduma zingine zinazopatikana katika simu.

END TO END ENCRYPTION INAFANYAJE KAZI?
Kama mtumaji na mpokeaji wame Update katika Whatsapp mpya basi Maongezi yao yatakuwa ni ya siri kupitia huduma hiyo ya End to End Encryption.

Huduma hiyo ambayo inatumiwa na Whatsapp ni Public key encryption: hii inakuwa ili uweze kumtumia ujumbe mtumiaji B lazima ujumbe wa mtumiaji A uombe nywila kwa server za Whatsapp na kufanya ujumbe wa mtumiaji A kufunga ujumbe wake na wa mtumiaji B.

Vilevile huduma hii mpya haichagui aina ya simu, iwe ni Android, Iphone, Windows phone hata zile simu ambazo ni za kizamani bado jumbe zao za picha, video, sauti na simu zitakuwa salama wa hali ya juu bila kudukuliwa.

KWANINI HUDUMA HII IMEWEKWA KTIKA WHATSAPP?

Huduma hii imewekwa katika mtandao wa Whatsapp kwasababu Mmiliki wa mtandao wa Whatsapp  JAN KOUM, alikuwa ni miongoni mwawatu ambao walikuwa mahakamani kuitetea kampuni ya Apple juu ya sakata na Serikali kuitaka kampuni hiyo itoe neno siri ambalo Apple iliweka katika simu zao tangia mwaka 2013.

Lakini Bado watumiaji wa huduma hii wanajiuliza kwanini imewekwa huduma hii?swali ambalo linaishia kujijibu wenyewe ni kwamba ni sababu ya ki usalama zaidi na bado Serikali huko nchini Marekani inazungumzia swala hili ni kwamba itakuwa chachu ya Magaidi kufanya mambo yao kwa huru kama huduma hizi zikiendelea katika mitandao ya kijamii.
Security

Wewe unalizingumziaje swala hili la kampuni ya Whatsapp kuweka huduma hii kwa watumiaji wake ili kulinda jumbe za watumiaji wake

0 comments:

Post a Comment