SIKILIZA VIDEO ZA YOUTUBE BACKGROUND KUPITIA UTUNDU HUU KATIKA SMARTPHONE YAKO



Wengi tunatamani video ambazo tunazicheza katika Youtube ziwe zinaendelea huku nasisi tukiwa tunaendelea na vitu vingine katika simu zetu kama kuchart kucheza game bila video ya youtube kutoka au kuacha kucheza..vipi hapo twende sasa..

Ili uweze kufanya utundu huo katika Smartphone yako lazima uwe unatumia Browser ya Google Chrome katika simu yako na kisha unafuata hatua hizi

1:FUNGUA BROWSER YAKO YA GOOGLE CHROME
Fungua browser ya Google chrome katika Smartphone yako kisha search youtube.com ukishamaliza kutafuta youtube ikishafunguka tafuta video ya nyimbo unayoitaka.

2:CHEZA YA WIMBO AU KITU CHOCHOTE
Ukishatafuta video ambayo ungependa kuisikiliza background huku waendelea na vitu vingine katika simu yako 
Bonyeza play ili kucheza hiyo video, ikishaanza ipige stop, ukishapiga stop hiyo video utaona alama ya sauti juu ya notification center katika smartphooneyako
YouTube video running in background

Ikishatokea alama hiyo basi toka katika huo ukurasa wa youtube, ukiwa bado unatumia Google chrome search kitu kingine tena kisha rudi juu kubonyeza play katika alama ya sauti, hapo utaweza kusikiliza Video za youtube ukiwa Background.


Mwisho kabisa Huduma hii sio kila simu inaweza kukubali kutokana na Smartphone yeneywe ilivyotengenezwa
Unaweza jaribu katika simu yako kisha nijulishe kama kwako wewe huo utundu umekubali.

0 comments:

Post a Comment