Kupitia Kipindi cha 360 cha clouds Tv, mwanamuziki kutoka WCB, Harmonize amesema kuwa wazo la wimbo wake mpya wa Bado ulikuja baada ya kumuuliza Diamond platnumz ni mwanamke gani ambaye hatokuja kumsahau maishani.
Baada ya kupata wazo hilo kutoka kwa Diamond ndipo alipochukua hatua ya kuandaa wimbo huo wa Bado.
"Idea ilikuja siku nilikuwa na Diamond katika gari, nikamuliza Diamond kuna mwanamke gani ulimopenda sana hadi leo unashindwa kumsahau..akaniambia hakuna masihara kwenye mahusiano mimi ndio nikapata idea" alisema Harmonize.
"Nikaona kama sio Diamond peke yake ambaye amekutwa na mambo hayo katika mahusiano, hata mimi yalishanitokea, kwahiyo nikaanza kuandika nilivyoandika nikampatia producer akanipatia beat nichague....Diamond alivyorudi kutoka Nigeria nikamsikilisha akaikubali akasema ataingiza verse ya pili" alimalizia Harmonize.
0 comments:
Post a Comment