Tukirudi nyuma Mwaka jana November Kampuni ya Google ilitangaza njia mpya ambayo unaweza kutest application kabla hujaipakia(Download) na Mwaka huu wa 2016 wametuletea tena Huduma nyingine ambayo unaweza kuijaribu Game kabla hujaidownload.
Watumiaji wa Simu za android kupitia Google search wataweza Kuijaribu game kwa kuicheza kabla ya kudownload kwa kutumia njia mpya inayoitwa Search trial Run ads.
Mtumiaji ili kuweza kujaribu huduma hiyo lazima awe katika network yenye kasi ambapo nazungumzia 4G au uwe na huduma ya Wireless hapo ndipo utaweza kutafuta Game unayoitaji kupitia Google search bar katika android yako baada ya hapo utaletewa option ambayo itakuwa ni TRY na Install.
Huduma hii itasaidia kwasababu unaweza kudownload game kumbe halikuwa zuri, kwahiyo Gamer sasa atakuwa na uwezo wa kulicheza Game kwa dakika hadi 10 ambazo zitamfanya kudownload au kuachana nalo na kutafuta Game nyingine.
Tazama mfano wa Jinsi ya kutumia search bar ya Google kujaribu Game kabla ya kuidownload
0 comments:
Post a Comment