Serikali ya Tanzania kupitia Bodi yake ya Sukari jana March 8, ilitangaza viwango vipya vya Bei ya sukari nchini vinavyoanza kutumika kuanzia sasa, Akiongea na waandishi wa Hbari Mkurugenzi wa Bodi ya Sukari nchini Henry Semwanza alisema
"Serikali, kupitia bodi ya Sukari Tanzania, inawaarifu wananchi wote kuwa bei ya rejareja ya sukari sasa itakuwa sh. 1,800 kwa kilo moja"
"wafanyabiashara wote wanapaswa kuzingatia agizo hili, pamoja na kuhakikisha kuwa sukari inaendelea kusambazwa na kuuzwa kwa wananchi bila kuihodhi‘
"Maafisa biashara wa mikoa na wilaya watafuatilia na kusimamia utekelezaji wa agizo kuhusu bei elekezi ya sukari, na hawatasita kuchukua hatua stahiki za kisheria kwa wale watakaobainika kupandisha bei ya bidhaa hiyo" Alisema Henry
0 comments:
Post a Comment