Watu 6 wamejeruhiwa katika mlipuko uliotokea katika uwanja wa ndege ulioko mjini Beledweyne nchini Somalia.
2 kati ya wale waliojeruhiwa ni maafisa wa polisi huku wengine wakiwa raia.
Bomu hilo linaaminika kuwa lilikuwa limetegwa ndani ya kipakatilishi (laptop).
Mtu aliyekuwa ameibeba bomu hilo alikuwa anajaribu kuingia katika eneo salama katika eneo la upekuzi la Beledweyne takriban kilomita 325km nje ya Mogadishu.
0 comments:
Post a Comment