VIRUSI VYA ZIKA VINASABABISHA KUPOOZA




Utafiti mpya,umetoa ushahidi kuonyesha kwamba virusi vya Zika vinaweza kuathiri vibaya kinga ya mwili.Utafiti huo ulifanywa miongoni mwa watu waliougua Zika miaka miwili iliyopita eneo moja la Ufaransa.


Iligunduliwa baadhi ya wagonjwa walipooza na hata baadhi wakafariki dunia kutokana na maambukizi ya Zika.
Virusi hivyo ambavyo vimesambaa kwa kasi kanda ya Amerika Kusini vimelaumiwa kusababisha dosari za kimaumbile hasa ukuaji wa ubongo kwa watoto wanaozaliwa.
Utafiti mpya umechapishwa na jarida la afya la Lancet

0 comments:

Post a Comment