Msimu huu wa Tuzo za Oscar Award hakuna mtu mweusi ambaye yumo katika nafasi za kuwania tuzo hizo ambazo hufanyika kila Mwaka.
Mwigizaji Idris Elba, aliyeteuliwa kupigania tuzo ya Bafta wiki iliyopita kutokana na uigizaji wake katika Beasts of No Nation hakuwa na nafasi.
Will Smith aliyemwigiza Dkt Bennet Omalu katika Concussion na Jason Mitchell aliyemwigiza Eazy E katika Straight Outta Compton pia hawamo.
Badala yake, filamu ya Straight Outta Compton, imependekezwa kwa ubunifu hii ikiwa na maana kwamba waliotunga hadithi hiyo, ambao ni Wazungu, ndio watakaopigania tuzo pekee.
Mwaka jana, kitambulisha mada #Oscarssowhite kilivuma mtandaoni baadaya waigizaji weusi kutoteuliwa kupigania tuzo hizo, na mwaka huu tena kinavuma mtandaoni.
Mtangazaji Chris Rock, ambaye ni mtu mweusi, ndiye pekee atakayewakilisha ulimwengu wa watu weusi katika tuzo za mwaka huu ambazo washindi watatangazwa tarehe 28 Februari.
Watu weusi ni asilimia 2 pekee kati ya jumla ya watu wanaopiga kura, kwa mujibu wa tovuti ya habari za burudani ya Rollingout.
0 comments:
Post a Comment