ANDY CARROL NJE WIKI SITA



Mshambuliaji wa West Ham Andy Carroll huenda akakaa nje kwa muda wa wiki sita baada ya kuumia misuli ya paja.Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 aliondolewa uwanjani baada ya kucheza dakika 15 pekee mechi dhidi ya Bournemouth, ambayo walishinda 3-1.
Carroll, 27, alikuwa amewafungia West Ham mabao mawili katika mechi zake nne za majuzi zaidi baada ya kurudi kucheza Septemba 2015.
Kabla ya hapo, alikuwa amekaa miezi saba nje baada ya kufanyiwa upasuaji kwenye goti lake.

0 comments:

Post a Comment