Kupitia Mtandao wa BBC umeeleza kuwa
Mbinu mpya ya kusafirisha data ambayo hutumia mwangaza badala ya mawimbi ya radio imejaribiwa.
Li-fi ina uwezo wa kumfanya mtumiaji kupata huduma ya mtandao mara 100 zaidi ya Wi-Fi na hutoa kasi ya hadi Gigabait moja kwa kila sekunde.
Li-Fi inahitaji mwangaza kama vile wa glopu,huduma ya mtandao na sensa ya picha
Ilijaribiwa wiki hii na Velmenni mjini Tallinn Estonia.
Velminni ilitumia glopu ya li-fi inayoweza kusafirisha data kwa kasi ya Gigabait moja kwa sekunde.
Jaribio la maabara limeonyesha kuwa li-fi ina kasi ya hadi Gigabait 224 kwa sekunde.
Ilijaribiwa katika afisi ili kuwasaidia wafanyikazi kupata huduma ya mtandao na katika kiwanda ambapo iliweka mwangaza.
0 comments:
Post a Comment