TWITTER IMEBADILI "FAVORITES" KWENDA KWENYE "LIKE"

Mtandao wa kijamii wa Twitter umebadilisha ile nembo ya nyota ambayo ilikuwa inatumika kama "Favorite" na kuweka nembo ya Kopa ambayo itatumika kama "Like".


Kampuni hiyo imeamua kuweka nembo hiyo ya kopa kwasababu ni nembo ambayo ulimwengu mzima inafahamu maana halisi, kopa huwa inaashiria upendo, furaha, mapenzi na itasaidia kujiunganisha na watu tofauti Duniani kote.



Kubadilishwa huko kutoka kwa nembo ya Nyota kuelekea ya Kopa, italetwa mda sio mrefu kwa wale watumiaji wa twitter kupitia Android, ios, Windows phone pamoja na wale wanaotumia computer.

0 comments:

Post a Comment