Mwanadada machachari kwenye tasnia ya muziki wa bongo fleva na vilevile Kinara wa tuzo ya Best Female East Africa kutoka kwenye mashindano ya Afrimma, Vanessa mdee amekuwa gumzo hivi sasa pamoja na video yake ya "Never ever" iliyoonyeshwa rasmi kwenye luninga ya Trace tv kabla ya luninga za kibongo.
Kwa mujibu wa kurasa ya instagram ya cloudsfmtz imesema video hiyo imemgharimu Vanessa dola za kimarekani elfu 20 ambazo ni sawa na zaidi ya shilingi Mil.40
Video hiyo ambayo imetengenezwa na Director Maarufu ambaye anazidi kujinyakulia umaarufu Afrika ya mashariki, Justin Campos wa Gorilla Films.
Mpaka sasa mwanadada Vanessa Mdee na video yake hiyo ya "Never ever" imeshafikisha viewer 80,000 toka ilipowekwa youtube ambapo mpaka sasa inasiku nne tu.
0 comments:
Post a Comment