Tecno hawako nyuma kwa wateja wao, na wametuletea simu yao mpya na yenye sifa za kisasa zaidi.
Simu hiyo inayoitwa Tecno phantom 5 ambayo ni mabadiliko makubwa kwa simu za Tecno, kwani Phantom 5 imekuja na uwezo mpya wa kufungua simu yako kwa kutumia kidole chako, kwa kuiegesha kwenye kitufe ambacho kinasaidia kufungua simu yako bila ya kutumia password.
Vilevile simu hiyo imekuja ikiwa na Android ya kisasa ambayo ni Android lollipo, yenye kasi na kufanya simu inakuwa nyepesi na kufanya vitu vingi kwa wakati mmoja bila ya simu kukwama kwama,
Ahsante kwa 32GB memory ya ndani ambayo unaweza kuhifadhi vitu vingi bila ya memory kujaa huku pia simunhiyo inakupa nafasi nyingine ya kuweka memory card ambayo inauwezo wa 64gb.
Kwa upande wa Kamera Phantom 5 inauwezo mzuri wa kuchukua picha kutokana na uweo wa kioo kuwa na Hd screen, c
kamera ya nyuma ina megapixel 13, huku kamera ya mbele ikiwa na megapixel 8 ambayo ni nzuri sana kwa kuchukua selfi bila ya wasiwasi.
Phantom inakupa speed ya kisasa zaidi ya mtandao amabayo ni 4G LTE,inasaidia kupakua vitu vingi kwa speed ya hali ya juu.
0 comments:
Post a Comment