Rapper kutoka New york 50cent anasema mziki mzuri unakuja wiki hii.
50 cent aliiachia cover art ya project yake jana katika kurasa yake ya instagram ikimwonesha msanii huyo ametokea kwenye rangi ya black and white huku akiwa amevalia mzula, chini ya hiyo picha ndio imeandikwa "Kanan Tape" ambayo ndiyo project yake itakayo kuwa na nyimbo 8.
Kabla ya kupost hiyo picha inayozungumzia kanan Tape, msanii huyo alikuwa kishaanza kutoa mfululizo wa video na picha kwa ajili ya kutangaza Tape yake.
The Kanan Tape imetokana na jina analotumia 50 cent "Kanan" kwenye tamthilia inayoitwa Power ambayo pia yeye ndiye producer wa hiyo series.
Bado hajaweka wazi tape hiyo ataitoa lini.
0 comments:
Post a Comment