MSTAA WA ZAMANI WA MAN UNITED KURUDI DIMBANI NOVEMBER 14 MWAKA HUU



Mastaa wa soka wa zamani watarudi dimbani kucheza katika mechi ya pamoja November 14 2015 katika dimba la Old Trafford. Miongoni mastaa wa zamani wa soka watakokuwepo katika kikosi cha timu hiyo ni David Beckham ambapo watacheza mchezo kwa ajili ya kuchangisha fedha katika mfuko wa UNICEF.
Beckham ambaye atakuwa nahodha wa kikosi hicho atajumuika pamoja na mastaa wenzake wa zamani kama Ryan GiggsPaul ScholesNicky Butt na Phil Neville na mastaa wote wa zamani wa Man United. Lakini upande wa timu ya David Beckhamatajumuika na wachezaji wenzake wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza kama Rio FerdinandSol CampbellAshley ColeDavid Seaman na Jamie Carragher.

Mastaa wa zamani wa Man United mara ya mwisho kucheza mechi ya pamoja ilikuwa mwaka 2011 katika mechi kwa ajili ya heshima kwa Gary Neville. Lakini kwa timu pinzani itakuwa na mchezaji wa zamani wa Real Madrid Zinedine ZidaneRonaldinhoLuis FigoCafuFabio CannavaroAlessandro NestaEdwin van der Sar na Patrick Vieira, kwa upande wa Gary Neville bado hajathibitisha kama atakuwa sehemu ya mchezo huo.

0 comments:

Post a Comment