KAAMPUNI YA SAMSUNG WAMEKUJA NA TABLET YENYE SCREEN KUBWA YA INCH 18.4 INAYOITWA "GALAXY VIEW"

Samsung Galaxy View

Kama Tablet yenye Screen kubwa ndio mpango mzima, Naweza nikasema sasa hii ni bonge la Tablet ambayo hatujawwahi kuona. Tablet hii kutoka Samsung imepewa jina la Galaxy view na kioo cha inch 18.4, yaani 18.4 inches kona kwa kona ya display yake. Kuhusu bei yake na je itatolewa lini kwa ajili ya mauzo? Bado kampuni ya Samsung haijasema chochote, ila kwa hichi kioo, bei lazima iwe kubwa kidogo.

Samsung wanatuambia kuwa uwezo wa screen hiyo umewekwa kwa ajili ya kuangalia movie, Tv series ukiwa nyumbani na familia.
resolution ya kioo hicho ni 1920*1080, huku procesor yake ikiwa na uwezo wa Octa core 1.6



Tablet hiyo ina mfumo uendeshaji wa Android 5.1 Lollipop na kuhusu swala la kudumu na betri, samsung wamesibitisha kuwa itakuwa na uwezo wa kukaa masaa 8 ukiwa unatizama video na uwezo wa kuhifadhi vitu wa ndani unatofautina, unaweza kupata ikiwa na 64GB na 32GB na vilevile mtumiaji utakuwa na uwezo wa kuweka memory card.



0 comments:

Post a Comment